MAHAFALI YA 29 YA CHUO CHA UKUTUBI NA UHIFADHI NYARAKA (SLADS)
23 11, 2023
Mkuu wa Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka yaani School of Library Archives and Documentation Studies (SLADS) kilichopo Bagamoyo na Dar es salaam, anapenda kuwakaribisha wahitimu wote wa mwaka 2022/2023 wa ngazi ya Stashahada (NTA 6) katika mahafali ya 29 ya Chuo hicho yatakayofanyika tarehe 25 mwezi Novemba, 2023 siku ya Jumamosi kuanzia saa tatu asubuhi chuoni Bagamoyo, mkoani Pwani.