Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa

CSSD

Divisheni ya Watoto na Shule (CSSD) hutoa huduma kwa watoto na wanafunzi na pia inahusika kutoa mwongozo katika uanzishaji wa maktaba za shule na vyuo, pia kutembelea shule kuanzia za awali, msingi na sekondari.

Divisheni imegawanyika katika vitengo vifuatavyo:-
•    check point (ukaguzi)
•    registration ( uandikishaji)
•    Issue desk and schools ( Uazimishaji)
•    Reference (huduma rejea)
•    Multmedia resources center( kitengo cha watoto wadogo )

MADHUMUNI
•    Kutoa huduma za maktaba kwa watoto kuanzia shule za chekechea hadi kidato cha sita na taasisi zingine zinazohusika na watoto.
•    Kuhamasisha watoto na vijana kupenda kujisomea na kujua umuhimu wa maktaba pamoja na kuitumia kwa kujielimisha.
•    Kutoa ushauri na miongozo kwa shule, na taasisi za watoto na jinsi ya kuwafanya watoto wapende kujisomea pia kuanzisha maktaba, kuziboresha na kuziendeleza.
•    kuhamasisha matumizi ya kompyuta na intaneti kwa watoto na vijana ili waweze kwenda sambamba na matumizi ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na madhara ya kuitumia vibaya teknolojia hiyo.

•    Kutembelea shule ili kuhamasisha walimu na wanafunzi wajenge utamaduni wa kujisomea na pia waendeleze maktaba za shule na kuzitumia maktaba hizo.
HUDUMA
Divisheni inatoa huduma zifuatazo:-
•    Uazimishaji wa vitabu kwa kusoma ndani na nje ya maktaba.
•    Uazimishaji wa vitabu kwa maktaba za shule.
•    Huduma ya kutembelea shule taasisi na jamii kwa ujumla (outrich programe) kutangaza huduma zitolewazo maktaba na kukagua maktaba zao.
•    Kushauri wasomaji kuhusu utumiaji wa maktaba na usomaji mzuri wa vitabu.
•    Kuandaa matamasha mbali mbali kwa ajili ya watoto 
•    Uandikishaji wa wanachama wapya na wale wa zamani (renewals) kuanzia shule za awali hadi sekondari.
•    Huduma endelevu “Multimedia resource Centre” (michezo mbalimbali ya watoto, hadithi, sanaa na nyingine nyingi)
•    Kuanzisha klabu mbalimbali na kuziendeleza kwa mfano ya usomaji, mazingira, midahalo, kazi za mikono na nyinginezo.


KUJIUNGA NA MAKTABA:
Watu wote wanakaribishwa kujiunga na kutumia maktaba kwa utaratibu ufuatao;

UANACHAMA WA MWAKA (WANAFUNZI WA SEKONDARI)
Kwa wanafunzi wa sekondari Ada ya uanachamawa wa kudumu  inatolewa kwa mwaka, kiasi cha shilingi elfu saba (7,000)/- kwa watanzania na USD 25.00 kwa wasio watanzania.

UANACHAMA WA MUDA (MWANAFUNZI WA SEKONDARI) 
Kwa wanafunzi wa sekondari Ada ya uanachamawa wa muda  inatolewa siku, kiasi cha shilingi elfu moja (1,000)/- kwa siku kwa watanzania na USD 2.00 kwa wasio watanzania.


UANACHAMA WA MWAKA (SHULE YA MSINGI NA AWALI)
Mtumiaj wa kudumu anachangia shilingi (elfu tano) 5,000/-kwa Mtanzania na USD 20.00 kwa asiye mtanzania


UANACHAMA WA MUDA (SHULE YA MSINGI NA AWALI)
Mwanachama wa muda ni mwanachama ambaye anatumia maktaba kwa siku. Mwanachama wa aina hii hchangia shilingi elfu moja kwa siku kwa Mtanzania, na asiye Mtanzania huchangia USD 2.00


UANACHAMA TAASISI NA MASHULE 
Shule au Taasisi hujiunga na kuchangia ada ya uanachama shilingi laki moja  (100,000/-) kwa mwaka


FAINI/ FIDIA YA UCHELEWESHAJI, UPOTEVU NA UHARIBIFU WA KITABU.
Endapo kuna uhafribifu, upotevu, ucheleweshaji wa kurudisha vitabu kwa muda uliopangwa, mtumiaji wa maktaba atalipa Faini /fidia ya ucheleweshaji ,upotevu  na uharibifu wa kitabu kama ifuatavyo.

•    Upotevu wa kitambulisho cha maktaba TSHs 2000.00
•    Upotevu wa tiketi  ya  kuazimia vitabu TSHs 2,000.00
•    Upotevu wa fomu  ya uanachama  TSHs 2,000.00
•    Kuchelewesha kitabu ( overdue charges) baada ya siku 14 kila siku  inayoongezeka itatozwa faini ya tsh 500.00
•    Kitabu kilichopotea kwa gharama halisi kwa wakati huo,