Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa

NBA

Kitengo cha Bibliografia ya Taifa ni  sehemu ya Maktaba ya Taifa ambayo inatekeleza  majukumu yafuatayo:

•    Kuelimisha wachapishaji wa ndani juu ya namna bora ya kuchapisha machapisho kwa kushirikiana na wachapishaji kuona namna ya kuchapisha machapisho yenye maudhui ya kitaifa na utamaduni wa kitanzania.
•    Kuwaunganisha wachapishaji kupitia uwasilishwaji wa machapisho kwa mujibu wa sheria (Legal Deposit)
•    Kutoa namba ya utambulisho wa machapisho ISBN na ISSN kama wakala wa kimataifa ya Namba hizi nchini kisheria.

Utoaji wa namba za tambulisho za machapisho yaani ISBN (Namba tambulisho ya kitabu) pamoja na ISSN (namba tambulisho ya majarida na magazeti).Namba hizi hutolewa katika kila chapisho la mwandishi.

Faida ya kuwa na ISBN katika chapisho 
1.    ISBN ni namba tambulisho ya kitabu ambayo hutumika na wachapishaji,waandishi,maktaba,wauzaji wa vitabu na wote wanahohusika na usambazaji na uhifadhi wa kumbukumbu.
2.    ISBN inatofautisha matoleo ya machapisho (edition)pamoja na majina ya vitabu.
3.    Ni namba tambulisho inayotumika kutofautisha kazi 

Nani anapaswa kupewa ISBN?
Mara nyingi mchapishaji ndiye anayepatiwa ISBN, lakini kwa lengo la ISBN mchapishaji anaweza kuwa Kampuni, Taasisi, Kikundi cha watu au mtu yeyote ambaye yupo tayari kuingia gharama katika uchapishaji.

Machapisho gani yanapewa ISBN?
1.    Kitabu
2.    Vitabu vya nukta nundu
3.    Vitabu mtandao
4.    Machapisho ambayo haya chapishwi kila baada ya muda Fulani mfano kila siku,kila wiki.
5.    Software za mafundisho ya kielimu
6.    Atlas

Ni mabadiliko gani yanalazimika kuwekwa ISBN mpya?
i.    Endapo kitabu kimebadilishwa jina au kuongezwa maneno kwenye jina la kitabu hicho(change title)
ii.    Toleo jipya la kitabu mfano toleo la pili,tatu na kuendelea.
iii.    Toleo la kielectronikali (ebooks) kila fomati inapewa ISBN namba yake mfano PDF, WORD,na kadhalika.
iv.    Lugha tofauti , lakini kichwa cha habari ni moja kila lugha itapewa ISBN yake.

ISSN ni namba tambulisho ambazo hutumika katika magazeti   ,majarida  au machapisho yoyote ambayo huchapishwa mara kwa mara mfano kila siku,kila wiki,kila baada ya miezi mitatu,kwa mwaka mara mbili au kwa mwaka mara moja.

Ni machapisho gani hupewa ISSN?
1.    magazeti
2.    majarida
3.    machapisho ya mwaka kama vile,directory na ripoti
4.    kanzidata
5.    blog
•    Kazi ya ISSN ni ipi?

Ni utambuzi wa chapisho.

Utoaji wa BARCODE ambao huambatana na namba za (ISBN) Huduma hii ya BARCODE NI BURE  baada ya kuwa mwanachama wa ISBN.