Ujenzi
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania imenufaika tena na fedha za maendeleo kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Katika mwaka wa fedha 2020/2021 kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo, kiasi cha shilingi Bilioni kumi na milioni mia tano (TZS 10,500,000,000) zilitengwa kwa ajili ya miradi kadhaa itakayotekelezwa.
Aidha, katika fedha hizo kuna fedha za ukarabati, ujenzi na miradi mingine ya Maktaba, ambapo Jengo la Makao Makuu ya Maktaba Dar es Salaam limetengewa kiasi cha shilingi Bilioni tatu (TZS 3 Bil.) kwa ajili ya Ukarabati.
Kwa upande mwingine, Maktaba mbili zinatarajiwa kujengwa ikiwemo Maktaba ya Kumbukumbu ya JPM Wilayani Chato itakayogharimu kiasi cha shilingi Bilioni tatu na nusu (3.5 Bil.) ambapo makabidhiano ya Nyaraka za ujenzi na eneo yalishafanyika tarehe 14 Julai 2022, pamoja na Maktaba ya Mkoa wa Arusha iliyotengewa kiasi cha shilingi Bilioni tano (TZS 5 Bil.)
Vilevile katika fedha hizi, kuna fedha za miradi ya Maktaba Mtandao kiasi cha shilingi bilioni mbili (2 bil.) na manunuzi ya samani na vifaa vya TEHAMA kiasi cha shilingi Bilioni moja na nusu (TZS 1.5 Bil.).