Ukarabati
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) imenufaika na fedha za ukarabati kupitia mradi wa ESPJ uliopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo ndio Wizara mama ya TLSB.
Kupitia mradi huo, Maktaba nane (8) za Mikoa ambazo ni; Maktaba ya Mkoa wa Iringa, Kilimanjaro, Tabora, Kigoma, Morogoro, Rukwa, Kagera na Ruvuma zimenufaika na fedha hizo za ukarabati.
Aidha, Maktaba sita (6), zimekamilika na zinatoa huduma kwa wananchi lakini Maktaba mbili (2) ambazo ni Maktaba ya Mkoa wa Kigoma na Maktaba ya Mkoa wa Ruvuma hazijakamilika ukarabati wake mpaka sasa. Sababu zilizopelekea Maktaba hiyo kutokamilika kwa wakati ni upungufu wa fedha kutokana na kubadilisha dhana ya ukarabati na kuwa ujenzi sababu ya uchakavu wa jengo hayo.