Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa

Historia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) ni Taasisi ya Umma iliyopo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Taasisi hii ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 39 ya mwaka 1963 ikijulikana kama Bodi ya Huduma za Maktaba Tanganyika.

 

Mwaka 1975, Sheria hiyo ilirekebishwa ambapo Sheria mpya ya Bunge Namba 6 ya mwaka 1975 iliundwa na kupelekea jina la Taasisi kubadilika kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanganyika na kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania.

Lengo kuu la kuundwa kwa TLSB lilikuwa kutoa fursa kwa wananchi wote bila ubaguzi wa aina yoyote, kutumia Maktaba za Umma ili kujipatia elimu, maarifa na taarifa mbalimbali zitakazowasaidia katika kujikwamua kutoka katika umasikini na ujinga na pia kupata burudani na kudumisha utamaduni.