Nini lengo la kuundwa kwa TLSB?
Lengo kuu la kuundwa kwa TLSB lilikuwa kutoa fursa kwa wananchi wote bila ubaguzi wa aina yoyote, kutumia Maktaba za Umma ili kujipatia elimu, maarifa na taarifa mbalimbali zitakazowasaidia katika kujikwamua kutoka katika umasikini na ujinga na pia kupata burudani na kudumisha utamaduni.