Pichani: Menejimenti ya TLSB na Maktaba ya Jamii Bustani, Rombo Kilimanjaro, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao maalum kilichofanyika tarehe 31 Julai, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano TLSB Makao Makuu Dar es Salaam, kikao hicho ni hatua muhimu kuelekea uzinduzi wa Maktaba hiyo utakaofanyika hivi karibuni. Kutoka Kulia waliokaa ni Ndug. Fidelis Swai Mjumbe wa Menejimenti ya Maktaba ya Bustani, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba Dkt. Rehema Ndumbaro (Katikati) na kulia ni ndug. Romani Urassa ambaye pia ni Mjumbe wa Menejimenti ya Maktaba ya Jamii Bustani. Waliosimama ni Menejimenti ya TLSB.