Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA KUHUSU HUDUMA ZA MAKTABA TAMASHA LA VITABU NA USOMAJI
service image

KONGAMANO LA NNE LA KITAIFA KUHUSU HUDUMA ZA MAKTABA TAMASHA LA VITABU NA USOMAJI

Tuesday Oct 20, 2026

07:00AM-18:00PM

Maktaba Kuu ya Taifa Posta - Dar es Salaam

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) inawakaribisha kwenye Kongamano la Nne la Kitaifa kuhusu Huduma za Maktaba, Tamasha la Vitabu na Usomaji, litakalofanyika tarehe 20–22 Oktoba 2026 katika viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa, Posta, Dar es Salaam. Kongamano hilo litakuwa na mada kuu “Maboresho ya Huduma za Maktaba kupitia Mageuzi ya Kidijitali, Kukuza Maarifa na Ujuzi kwa Maendeleo Endelevu,” pamoja na uzinduzi rasmi wa Mfumo Jumuishi wa Maktaba Mtandao ya Taifa (iNDLS), maonesho ya vitabu, mashindano ya usomaji kwa watoto na wanafunzi, pamoja na burudani mbalimbali. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda.  NYOTE MNAKARIBISHWA! #MaktabaKidijitaliNaUjuziKwaDira2050  

slot gacor