Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
KITUO CHA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO TUMBI WATEMBELEA MAKTABA YA TAIFA
18 Oct, 2025
service image
Walezi na Watoto 57 kutoka Kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto Tumbi, kilichopo chini ya Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani, wametembelea Maktaba ya Taifa Posta kujifunza umuhimu wa kusoma vitabu na kujionea mazingira ya kujifunzia kupitia maktaba leo tarehe 17 Oktoba,2025 . Wageni hao walipokelewa na mkuu wa kitengo cha watoto Bi. Mwajuma Rasuli, akiambatana na wakutubi wengine wa kitengo hicho, ambao waliwaonesha na kuwaeleza watoto kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kitengo hicho. Watoto walishiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo kuchora, kupaka rangi,michezo ya kuunganisha vifaa ili kutengeneza umbo la kitu na waliimba nyimbo za shule, ambazo zililenga kuwajengea ubunifu, ujasiri na furaha ya kujifunza katika mazingira rafiki. Ziara hiyo iliongozwa na Mkuu wa Kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto, Bi. Martha Anania, ikiambatana na walimu watano na wafanyakazi wawili wakiwa na lengo la kuwafunza watoto kwa vitendo jinsi maktaba inavyowawezesha kujifunza kwa njia bora na ya kuvutia angali wakiwa wadogo. Akizungumza mwishoni mwa ziara hiyo, Bi. Martha Anania aliishukuru TLSB kwa ukarimu na elimu waliyoitoa kwa watoto, akibainisha kuwa ziara hiyo imewachochea watoto kupenda kusoma na kutembelea maktaba mara kwa mara. Kwa upande wake, Bi. Mwajuma Rasuli amesema Maktaba ina jukumu la kukuza utamaduni wa kusoma kuanzia ngazi ya awali na kulea vizazi vinavyopenda kujiongezea maarifa.