Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
PROF. MUKANDALA ATETA NA WAJUMBE WAPYA WA BODI TLSB
29 Apr, 2025
service image
Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi TLSB wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuletea Bodi mafanikio kwani wamepewa dhamana kubwa na kuaminiwa kushika nafasi hizo. Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Bodi ya TLSB Prof. Rwekaza Mukandala wakati akiwakaribisha Wajumbe hao leo tarehe 10 Aprili, 2025 katika Mafunzo ya Wajumbe na Menejimenti yanayofanyika Ramada Resort, Dar es Salaam. Prof. Mukandala amewaagiza Wajumbe hao kuhakikisha wanashauri vyema na kuchangia mawazo yao ili kuwezesha bodi kusonga mbele. Kwa upande wa Menejimenti, Prof. Mukandala ametoa rai kushirikiana vyema na Wajumbe hao ili kwa pamoja watimize mipango na malengo ya Bodi. Pichani: Bodi ya Wakurugenzi TLSB katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Rwekaza Mukandala ( Aliyekaa katikati) leo tarehe 10 Aprili, 2025 katika hoteli ya Ramada, Dar es Salaam.