TLSB YAADHIMISHA MEI MOSI 2025
05 May, 2025
TLSB imeshiriki maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida tarehe 1 Mei, 2025.
Katika maadhimisho hayo, Watumishi wa TLSB Maktaba ya Mkoa wa Singida wameungana na maelfu ya Watumishi kutoka sekta mbalimbali nchini kuadhimisha siku hii muhimu kwao kwa kubeba mabango yenye jumbe mbalimbali na kupita mbele ya Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, katika hotuba yake kwa Wafanyakazi, Rais Samia ametangaza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kimeongezeka kutoka shillingi za Kitanzania 370,000 hadi shilingi 500,000 sawa na ongezeko la asilimia 35.1.
Kwa upande mwingine, Viongozi mbalimbali wamehudhuria Maadhimisho ya Mei Mosi katika viwanja vya Bombadia akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea aliyeambata na Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji Huduma za Maktaba Dkt. Rehema Ndumbaro na maafisa wengine kutoka TLSB Makao makuu Dar es Salaam.
Maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu "Uchaguzi Mkuu 2025, Utuletee viongozi wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiri".
Pichani: Watumishi wa TLSB Maktaba ya Mkoa Singida katika maadhimisho ya Mei Mosi ndani ya Viwanja vya Bombadia.
#TLSBUPDATES