Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
VITABU KUTOKA FAMILIA YA HAYATI CHRISTOPHER MWAIJONGA
28 Apr, 2025
service image
Bodi ya huduma za maktaba Tanzania (TLSB), imepokea vitabu zaidi ya 150 kutoka kwa familia ya marehemu Christopher Mwaijonga ya jijini Dar es salaam, tarehe 6 Februari 2024. Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TLSB katika mapokezi hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji Huduma za Maktaba Dkt. Rehema Ndumbaro, ameishukuru sana familia ya Hayati Christopher Mwaijonga kwa mchango huo wa vitabu. Aidha ameongeza kuwa, moja ya majukumu ya maktaba ya taifa ni kupokea, kukusanya na kusambaza huduma za maktaba kwa watumiaji wakiwemo wanachama kutoka taasisi za kiserikali, binafsi na maktaba za kijamii. “Vitabu hivi vitakuwa  msaada mkubwa sana kwa watumiaji wote  kwani kuvileta hapa hujahudumia Dar es salaam peke yake bali unahudumia Tanzania nzima ambapo tuna maktaba za mikoa 22 za wilaya 19 na tarafa 3, hivyo tuna mtandao wa maktaba 43.” Dkt.Ndumbaro ameeleza. Dkt.Ndumbaro pia amesema Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania inawajibu wa kusimamia uanzishaji na uendelezaji wa maktaba, pia inatoa ushauri kwa yeyote anayeanzisha maktaba. Akizungumza kwa niaba ya familia iliyotoa vitabu, Bi Irene Christopher Mwaijonga amesema marehemu baba yao alikua msomaji mzuri wa vitabu na alikusanya vitabu vingi vyenye maudhui mbalimbali. Kwa kutambua umuhimu wa kusoma vitabu familia ina muenzi kwa kuviweka maktaba ili wasomaji wengine wanufaike. “Sisi kama familia ya marehemu Christopher Mwaijonga tunaomba vitabu hivi vitumike ipasavyo na tunajua vitasaidia watu wengi kwa sababu sisi muda mwingine tunakaa na vitu ambavyo vina maarifa wanayohitaji watu wengine.” Vitabu vilivyokabidhiwa vina maudhui mbalimbali kama vile; Afya, idadi ya Watu, Mazingira, Watoto, Ukimwi na maudhui mengine mbalimbali.