Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
WAANDISHI WA VITABU WASISITIZWA KUJIFUNZA MATUMIZI YA AKILI MNEMBA (AI)
25 Nov, 2025
service image
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Dkt. Mboni Ruzegea, leo tarehe 25 Novemba 2025 ameongoza semina muhimu kwa wakutubi, waandishi wa vitabu, wachapishaji na wadau wa elimu, ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Vitabu yanayofanyika katika Viwanja vya Maktaba Kuu ya Taifa, jijini Dar es Salaam. Katika semina hiyo, Dkt. Mboni amesisitiza umuhimu wa wataalamu wa sekta ya vitabu na elimu kujifunza na kutumia teknolojia za Akili Mnemba (AI) ili kuboresha uzalishaji wa maarifa, utafiti, utunzaji wa taarifa na utoaji wa huduma za maktaba kwa ufanisi zaidi. Amesema kuwa matumizi ya AI yamekuwa chachu ya mageuzi duniani na kwamba wadau wa sekta ya elimu hawapaswi kuachwa nyuma. Aidha, Dkt. Mboni ameielezea maktaba kama nguzo kuu na kiini cha maarifa, akibainisha kuwa maendeleo ya elimu, uandishi na uchapishaji hayawezi kutenganishwa na uwepo wa maktaba imara zinazohifadhi, kusambaza na kukuza upatikanaji wa taarifa sahihi kwa jamii. Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Wachapishaji Tanzania (PATA) ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wadau waimarishe ujuzi na maarifa katika utoaji wa huduma na kazi zao za kila za kila siku, ikiwemo kuboresha mbinu za uandishi, uchapishaji na utoaji wa huduma za elimu kwa kutumia teknolojia za kisasa.