TANGAZO: Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea, atafanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuelezea Mafanikio na Mwelekeo wa Bodi katika Miaka Minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkutano huo utafanyika tarehe 28 Machi, 2025 katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano TLSB Makao Makuu, Dar es Salaam.